Arsenal walionyesha ubora wao kwa kuwatandika Porto kutoka Ureno mabao 5-0 kwenye mechi ya marudiano na ya kuwania tiketi ya kuingia robo fainali za kombe la kilabu bingwa barani Ulaya.
Mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika sehemu kadhaa nchini Morocco, imesababisha maafa na hasara kubwa. Takriban watu 10 wameripotiwa kuuawa kwenye mafuriko nchini humo.